Friday, June 28, 2013

Pistorius kufanya mazoezi kupunguza mawazo

South Africa's Oscar Pistorius starts his men's 400m round 1 heats at the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium August 4, 2012. REUTERS/Dylan Martinez (BRITAIN - Tags: OLYMPICS SPORT ATHLETICS TPX IMAGES OF THE DAY)
Oscar Pistorius anatarajia kuanza kufanya mazoezi mepesi ili kumsaidia kupunguza mawazo ya kesi yake ya mauaji ya mchumba wake Reeva Steenkamp. Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Pistorius imesema mwanariadha huyo anayetumia miguu ya kubandikwa, ameamua kufanya mazoezi mepesi kwa saa chache kila wiki ili kujiandaa kiakili. Pistorius amesema hatashiriki katika mashindano yoyote mwaka huu wote wa 2013 ili kupata muda wa kushughulikia vyema kesi yake inayooenekana kuchukua muda mrefu. Kesi yake itaendelea Agosti 19, wakati waendesha mashitaka watakapoamua kama ana mashitaka ya kujibu au la, na tarehe ya kuanza rasmi kesi yake huenda ikawekwa mwezi Septemba au Oktoba. Pistorius mwenye umri wa miaka 26, mara ya kwanza alipopandishwa kizimbani alikanusha mauwaji dhidi ya Steenkamp, akisema alimpiga risasi kimakosa kwa sababu alidhani ni mwizi aliyeingia nyumbani kwake. Kama atapatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia, atakabiliwa na adhabu ya kifungo cha chini cha miaka 25 gerezani.

No comments:

Post a Comment