Monday, June 24, 2013

Guardiola akabidhiwa rasmi mikoba Bayern Munich

Pep GuardiolaKocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola leo amekabidhiwa rasmi mikoba ya Jupp Heynckes kuifundisha klabu Bayern Munich. Tukio hili la makabidhiano limefanyika leo mbele ya waandishi wa habari jijini Munich kwenye makao makuu ya klabu hiyo. Katika maongezi yake na waandishi wa habari Guardiola alisema 'ninajua mazingira yangu ya kazi, kwani ninaanza kazi kwenye wakati mgumu sana, wakati ambao ninatakiwa kuhakikisha kile alichokifanya kocha aliyepita nakitekeleza kama yeye au zaidi yake, lakini jambo hili kwangu sio gumu kwasababu nimeshapitia mazingira haya nikiwa Barcelona, hivyo hali hii sio ngeni kwangu. Vilevile, najua mashabiki wa Bayern Munich wanatarajia makubwa kutoka kwangu kwasababu wanajua mafanikio niliyopata nikiwa na Barcelona, naamini nitatimiza kiu yao'. Kabla ya kujiunga na Bayern, Guardiola aliweza kuingoza vyema klabu ya Barcelona na kufanikiwa kutwaa makombe 14 kwa miaka minne jambo ambalo ni historia hadi sasa ndani ya klabu hiyo. Mafanikio haya ndiyo ambayo washabiki wa Bayern Munich wanayataria kuyaona kwa timu yao ikiwemo pia kuwafundisha wachezaji wa Bayern Munich aina mpya ya kucheza mpira inayofanana na Barcelona. 

No comments:

Post a Comment