Monday, June 24, 2013

Nadal aweka historia kutolewa raundi ya kwanza

Bingwa wa Wimbledon mara mbili Rafael Nadal, leo ameushangaza ulimwengu wa tenesi baada ya kutolewa kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo kwa seti tatu mfululizo za 7-6, 7-6 na 6-4 dhidi ya Steve Darcis. Umati mkubwa wa mashabiki wa Nadal ulifurika kwenye kiwanja namba moja cha michuano hii ili kushuhudia mwanzo mzuri wa mchezaji huyo, lakini walijikuta wanapatwa na butwaa kubwa kuona bingwa huyo wa Wimbledon na French Open anatolewa kiurahisi na Steve ambaye ni mara yake ya kwanza kuingia raundi ya pili ya michuano hii. Matokeo haya yanamfanya Nadal kuacha njia nyepesi kwa mpinzani wake Roder Federer kushinda tena kombe hili kwa mara ya nane, jambo ambalo litamfanya Federer kuwa mchezaji pekee aliyechukua Wimbledon mara nyingi kuliko wote. 


 Rafael Nadal  Nadal
Resigned: Nadal's movement was well below par Sporting: Nadal congratulates Darcis on his win\
Picha ya kushoto inamuonesha Rafael Nadal akishangaa pasipo kuamini kilichotokea uwanjani baada ya kupigwa seti tatu mfululizo na Steve. Picha ya kulia inamuonesha Nadal akimpa mkono wa pongezi Steve baada ya mchezo kuisha 

Rafael Nadal Rafael Nadal
Nadal akiwaaga mashabiki wake kwa huzuni huku akiwa anatoka nje ya uwanja. Hii ni mara ya kwanza kwa Nadal kutolewa kwenye raundi ya kwanza Wimbledon. 

Celebration: Darcis accepts the applause from the crowd after his massive upset
Steve akishangilia baada ya mchezo kuisha

No comments:

Post a Comment