Saturday, June 22, 2013

Kesi ya Messi kukwepa kodi kutolewa hukumu Sept

Complications: Messi, shopping at Dolce and Gabbana in Milan, will pay the £3.4million tax fine
Juarez Veciana mwanasheria wa Lionel Messi amesema pesa anayodaiwa mteja wake italipwa kama kweli mahakama itathibitisha kuwa mchezaji huyo alikwepa kodi. Kesi hiyo itasikilizwa tena mwezi wa tisa kwa mara ya mwisho na mahakama itatoa maamuzi baada ya uchunguzi. Messi na baba yake wanadaiwa kukwepa kodi ya paundi mil 3.4 kuanzia mwaka 2007 hadi 2009 kutokana na kipato anachokipata mchezaji huyo kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali. Kama Messi atathibitika kukwepa kiasi hicho cha fedha atahukumiwa kwenda jela miaka sita au kulipa faini ya asilimia 150 ya kiasi anachodaiwa. 

No comments:

Post a Comment