Saturday, June 22, 2013

Luis Alberto atua Liverpool kwa ada ya paundi mil 6.8

Luis Alberto
Klabu ya Liverpool imemsajili rasmi mshambuliaji wa Sevilla Luis Alberto kwa ada ya paundi mil 6.8. Luis Alberto mwenye umri wa miaka 20 raia wa Hispania amesaini mkataba wa miaka minne hadi mwaka 2017. Msimu uliopita Luis Alberto alichezea Barcelona B kwa mkopo na alifanikiwa kufunga magoli 11 kati ya mechi 38 alizocheza. Alberto anaungana na Kolo Toure pamoja na Aspas ikiwa ni wachezaji ambao wameshasajiliwa na Liverpool hadi sasa kwa ajili ya msimu ujao.  

No comments:

Post a Comment