Monday, June 3, 2013

Mourinho ameshawasili London, anangojea kutangazwa

Back in England: Jose Mourinho is back in London ahead of his expected return to Chelsea
Jose Mourinho akiwa Heathrow Airport London jana mchana akitokea Hispania tayari kuanza kazi ya kuifundisha Chelsea. Taarifa zinasema muda wowote kuanzia sasa Mourinho atatangazwa rasmi na uongozi wa Chelsea kuwa kocha wa klabu hiyo. Katika maneno yake kuhusiana na kurudi Chelsea Mourinho alisema " nimerudi kwenye klabu ambayo napendwa zaidi, furaha yangu ni kuwa na Chelsea". Kurudi kwa Mourinho kwenye ligi ya Uingereza kutaleta ushindani mkubwa kwani historia ya Mourinho inaonesha hakai zaidi ya miaka miwili bila kushinda kombe la ligi, lakini pia izingatiwe kwamba klabu zote tatu za juu kwenye ligi yani Man utd, Man city na Chelsea zitakuwa na makocha wapya na kila kocha atapenda kuonesha uwezo wake hivyo ushandi wa kombe la ligi msimu ujao utakuwa mtamu sana.   

No comments:

Post a Comment