Monday, June 3, 2013

Neymar atambulishwa rasmi Barcelona

Hatimaye mshambuliaji mpya wa Barcelona Neymar Jr. ametambulishwa rasmi na klabu hiyo mbele ya washabiki wa Barcelona waliofurika katika uwanja wa Nou Camp. Neymar amejiunga na Barcelona akitokea Santos ya Brazil kwa paundi mil 50, leo amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Barcelona na baada ya hapa atarudi tena nchini Brazil kwenye timu ya taifa ambapo Brazil ipo kwenye maandalizi ya michuano ya Confederation cup inayotarajiwa kuanza Juni 15. Neymar amewasili leo asubuhi jijini Barcelona akitokea Brazil ambapo jana usiku alicheza kwenye mechi kati ya Brazil na England mechi iliyokwisha kwa droo ya goli 2-2. Neymar hajapewa namba bado anatarajiwa kupewa namba pindi akirudi kutoka kwenye timu ya taifa. Katika mahojiano yake ndani ya uwanja Neymar alisema "najisikia raha kuwa mchezaji wa Barcelona, ilikuwa ni ndoto yangu kwa muda mrefu, leo mara yangu ya kwanza kufika Barca lakini nimepapenda sana kama nilivyokuwa nawaza, mazingira yake mazuri sana, nimefurahi kuwa hapa na nitajituma niweze kuisaidia Barca, lakini pia nitamsaidia Messi kuwa mchezaji bora zaidi ya sasa".

FOTO: MIGUEL RUIZ-FCB.
FOTO: MIGUEL RUIZ-FCB.
Neymar apresentação Barcelona (Foto: AFP)
Neymar contract
Neymar

Video Neymar alipotambulishwa Nou Camp

No comments:

Post a Comment