Monday, June 24, 2013

Nik Wallenda aweka rekodi nyingine ya dunia


Daredevil Nik Wallenda ameweka rekodi nyingine duniani kwa kufanikiwa kuvuka kwa waya korongo kubwa duniani Grand Canyon lenye urefu wa mita 426.7 kwa kutumia dakika 22. Wallenda mwenye umri wa miaka 34, hii imekuwa ni mara yake ya pili kuweka rekodi ya dunia kuvuka makorongo kwa waya baada ya mwaka jana kuvuka maporokoko ya Niagara na kufanikiwa kuingia kwenye nafasi ya saba ndani ya kitabu cha rekodi za dunia Guinness. Wallenda alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliojitokeza kwenye tukio hilo alisema ‘nimefurahi kufanikiwa kuvuka Grand Canyon, kwani ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu, ila nilipata wakati mgumu sana katikati ya korongo kutokana na upepo mkali uliokuwa ukinipiga, lakini nilikuwa makini zaidi na kuelekeza fikra zangu kwenye njia hadi mwisho’. Angalia video hapo chini kuona tukio hili la kimaajabu  

No comments:

Post a Comment