Saturday, July 6, 2013

Chelsea na Man city vs PSG kumsajili Cavani

Cavani could be the latest big name to join PSG
Chelsea na Man city bado zinaendelea kupata upinzani mkali dhidi ya klabu tajiri PSG katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani. Raisi wa Napoli amethibitisha hayo kwa akisema ‘Cavani mwenyewe anapenda kwenda PSG kwasababu ameahidiwa kupewa mshahara wa Euro mil 8 kwa mwaka, vilevile, PSG wametoa ofa ya Euro mil 63 kumsajili mchezaji huyu, fedha ambazo ni nyingi kuzidi wengine, hatuwezi kusema Cavani ameshasajiliwa na PSG ila hadi sasa PSG wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsajili Cavani’. Chelsea na man city ndiyo klabu za mwanzo kutangaza kumsajili Cavani, na Chelsea walikuwa kwenye hatua za mwisho mwisho kumsajili mchezaji huyu, lakini mambo yalianza kubadilika pindi Rafa Benitez alivyochaguliwa kuwa kocha wa Napoli na kuanza kumshinikiza Cavani asihame, jambo ambalo lilipunguza nguvu ya Chelsea hadi PSG walipoingilia kati kwa kutoa dau kubwa zaidi. Kwa mujibu wa  Stefan Coerts mwandishi wa jarida la Goal, Cavani ameshasaini mkataba binafsi na PSG na imebakia klabu ya Napoli kuridhia ili Cavani ajiunge rasmi na PSG. 

No comments:

Post a Comment