Guus Hiddink kocha wa Anzhi Makhachkhala amejiuzulu ghafla kuifundisha klabu hiyo hii leo bila kutaja sababu yoyote akihusishwa kujiunga na Barcelona ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Tito Vilanova. Hiddink aliongeza mkataba wake mwezi uliopita kuifundisha Anzhi, lakini mwezi mmoja umepita ametangaza kujiuzulu bila kutaja sababu. Kitendo hiki kimehusishwa moja kwa moja na kocha huyu kujiunga na klabu ya Barcelona ambayo imetangaza kumtaja kocha mpya wa klabu hiyo kesho jumanne. Mbali ya Anzhi, Hiddink ameshawahi kuzifundisha klabu za Chelsea, Real Madrid na timu ya taifa ya Urusi. Nafasi ya Hiddink imezibwa na Rene Meulensteen aliyekuwa msaidizi wa Sir Alex. |
Monday, July 22, 2013
Hiddink ajiuzulu ghafla, ahusishwa na Barcelona
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment