Klabu ya Barcelona imeitolea nje ofa ya pili iliyotolewa na klabu ya Man utd kumsajili kiungo wake Cesc Fabregas. Man utd walituma ofa ya pili ya paundi mil 30 wikiendi iliyopita baada ya ofa ya kwanza ya paundi mil 25 kukataliwa. Taarifa kutoka kwa klabu ya Barcelona kama ilivyonukuliwa na gazeti la Espana inasema, klabu ya Barcelona haipo tayari kumuuza Cesc kwasababu ndiye mchezaji pekee aliyebakia kwenye benchi la klabu hiyo sehemu ya kiungo baada ya Thiago kuuzwa. ‘Cesc ndiye mchezaji atakayeweza kuziba mapengo ya Xavi na Iniesta pindi watakapokuwa majerehi, hivyo, kumuuza ni hatari kubwa kwani klabu itakuwa haina kiungo mbadala’. Mbali ya sababu hiyo, Espana pia imeeleza klabu ya Barcelona kwasasa ipo kwenye harakati ya kutafuta kocha mpya, hivyo uongozi wa klabu hiyo hauwezi kumuuza mchezaji ambaye anaweza kuhitajika na kocha mpya. |
Monday, July 22, 2013
Barcelona yaitolea nje tena Man utd usajili wa Cesc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment