Saturday, July 20, 2013

Je L'pool watakubali hii ofa? Higuain+£20m=Suarez

Klabu ya Real Madrid imejiandaa kutoa ofa nyingine kwa Liverpool ili kumsajili Luis Suarez. The Sun linaripoti kuwa, Real Madrid itatuma ofa ya paundi mil 20 pamoja na Gonzalo Higuain juu ili kumsajili Luis Suarez. Hii itakuwa ni ofa ya pili kwa Real Madrid kupeleka Liverpool baada ya ile ya kwanza kukataliwa. Ofa hii ya mara ya pili imeonesha kuikandamiza klabu ya Arsenal ambayo inawawinda wachezaji wote wawili Suarez na Higuain. Kama Liverpool watakubali ofa hii ya Real Madrid, ina maana Arsenal itakuwa imewakosa wachezaji wote wawili kwa mpigo. Arsenal wenyewe wametuma ofa ya mwisho ya paundi mil 40 kwa Liverpool ambayo imekataliwa baada ya kocha wa Liverpool Brendan Rodgers kusema Suarez hauzwi chini ya paundi mil 55. Hadi sasa ni klabu hizi mbili tu ambazo zinamuwania Suarez, na taarifa zinaonesha klabu itakayotoa pesa nyingi ndiyo itakayoweza kumsajili mchezaji huyu.  

No comments:

Post a Comment