Friday, July 19, 2013

Kocha wa Barcelona Tito Vilanova aachia ngazi

Tito Vilanova set to resign?
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova ametangaza kuachia ngazi kuifundisha klabu hiyo kwasababu ya maradhi. Rais wa klabu hiyo Sandro Rosell ametangaza rasmi taarifa hizi leo jioni baada ya mazoezi mbele ya wachezaji wa kalbu hiyo na waandishi wa habari. Rosell amesema Tito hataweza kuendelea kuifundisha klabu hiyo kutokana na maradhi ya kansa aliyonayo kuendelea kumsumbua, hivyo anapumzika ili aweza kupata matibabu. Kufuatia hali hii klabu ya Barcelona haitaweza kucheza mechi yake ya kirafiki iliyotarajiwa kuchezwa jumamosi hii nchini Poland hadi hapo itakapo tangazwa tena. Tito amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa tokea msimu uliopita na ilimchukua takribani miezi miwili kutibiwa akiwa Marekani   jambo ambalo liliathiri timu kwa kiasi fulani. Kuondoka kwake kuinaifanya klabu hiyo kuwa kwenye wakati mgumu kutafuta mrithi wake atakayeweza kuifundisha timu kwa kipindi kifupi kabla ya ligi kuanza. 

No comments:

Post a Comment