Monday, July 1, 2013

Obama kamfungulia njia Hasheem Thabeet

Rais wa Marekani Mh. Barack Obama katika maongezi yake na waandishi wa habari leo jioni, alimtaja Hasheem Thabeet ambaye ni mchezaji wa Kitanzania anayecheza NBA kwenye timu ya Oklahoma City Thunder nchini Marekani. Rais Obama alisema 'leo hatujapa muda wa kutosha mimi na Rais Kikwete kumuongelea Hasheem Thabeet, lakini tukipa muda nyakati zijazo tutaweza kumuongelea'. Kauli hii tu ya Rais Obama kumtaja Hasheem  bila hata kumuongelea kwa undani yeye na Rais Kikwete ni msaada tosha kwa mchezaji huyu wa Kitanzania kuzidi kujulikana zaidi na hata kumuwezesha kupata mikataba minono zaidi kwenye timu kubwa za NBA. Michezoupdates imethibisha hili muda mchache tu baada ya Rais Obama kumtaja, vyombo vingi vya habari vya kimataifa vilianza kumuongelea Hasheem na kuripoti habari hii. Baadhi ya vyombo hivi vya habari ni USA Today, NESN na ESPN ( kwa wale wanaopenda kusoma baadhi ya habari hizo wanaweza kubofya kwenye link hizi USA Today  na NESN. Watanzania tunazidi kung'ara, taratibu ndiyo mwendo, tutafika tu. 

No comments:

Post a Comment