Monday, July 1, 2013

Utani mwingine unaweza kujenga bifu hivi hivi

1372692595629 Brilliant Photoshop: Neymar kissed Sara Carbonero after Brazil beat Spain at Confederations Cup
Baada ya michuano ya kombe la mabara kuisha, picha hii ya kutengeneza imeenea kwenye vyombo vya habari duniani ikimuonesha mshambuliaji wa Brazil Neymar akimbusu Sara ambaye ni mchumba wa golikipa wa Hispania Casillas. Lengo kuu la picha hii ni kuonesha uonezi wa Neymar kwa Casillas kuanzia kiwanjani hadi kwa mpenzi wake. Baada ya kutoka picha hii baadhi ya watu walidhani ni ya kweli kutokana na utaalamu wa hali ya juu uliotumika kuunganisha, lakini kadri ya muda ulivyokwenda watu ndipo walipoanza kugundua kuwa sio ya kweli. Uhalisia wa picha hii ni picha iliyopo chini ambayo inamuonesha Casillas akimbusu Sara kwenye interview ya siku ambayo Hispania ilishinda kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini mwaka 2010. 
Hii ndiyo picha halisi ya Casillas akimbusu Sara. Picha hii ndiyo imetengezwa na kuifanya ionekane kuwa Neymar anambusu Sara.

Hii ndiyo Video ya tukio lenyewe Casillas akimbusu Sara (Sara ni mtangazaji wa TV, alikuwa akimhoji Casillas baada ya mechi kuisha mwaka 2010, ila Casillas alizidiwa na furaha akahisi yupo chumbani....) 

No comments:

Post a Comment