Tuesday, July 16, 2013

Rudisha nje mbio za Moscow kutokana na majeraha

Bingwa wa dunia, olimpiki na mshikilia rekodi ya ulimwengu katika mbio za mita 800 kwa wanaume Mkenya David Rudisha, amejiondoa kwenye mashindano yajayo ya dunia yatakayofanyika mjini Moscow, Urusi mwezi ujao. Kwa mujibu wa naibu makamu wa rais wa shirikisho la mchezo wa riadha nchini Kenya, David Okeyo amesema, Rudisha hatatetea taji lake mwaka huu kutokana na majeraha anayojiuguza. Okeyo amesema baada ya kushauriana na mwanariadha huyo pamoja na makocha wake, imebainika kuwa Rudisha bado anauguza majeraha na haitakuwa vyema kushiriki katika mashindano hayo kwa kuwa inaweza kuhatarisha zaidi jeraha hilo.

No comments:

Post a Comment