Tuesday, July 16, 2013

Fabregas aitolea nje klabu ya Manchester United

United front? Fabregas is a target for new United boss David Moyes
Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas amesema hana nia yoyote ya kuihama klabu hiyo na kurejea tena nchini England. Maneno haya yamesemwa na kocha wa Barcelona Tito Vilanova wakati anaongea na waandishi wa habari baada ya mazoezi ya klabu hiyo kuanza. ''Ni ishara nzuri kwa klabu yoyote kupata maombi kutoka kwa vilabu vingine vinavyotaka kuwasajili wachezaji wake, lakini Fabregas amesema anataka kubakia Barca'' Vilanova ameliongelea jambo hili kufuatia ofa ya Manchester United iliyowasilishwa siku ya Jumatatu yenye ombi la kutaka kumasajili nahodha huyo wa zamani wa Arsenal kwa kitita cha paundi mil 25, lakini Vilanova amesema mchezaji huyo anataka kubakia nchini Uhispania kwa sasa. 

No comments:

Post a Comment