Mshambuliaji wa Arsenal, Lukas Podolski amesema haogopi
kukosa namba kweye kikosi cha kwanza hata kama Gonzalo Higuain atajiunga na
klabu hiyo. Podolski ameyasema hayo alipokuwa akiongea na The Sun akisema ‘wakati wote ni vyema kuona wachezaji wazuri wanasajiliwa, mimi sina wasiwasi
wowote kwasababu najiamini ni mchezaji mwenye nguvu na uwezo mzuri. Wachezaji wazuri
wakija nafurahi, kwasababu nitacheza vizuri zaidi. Mambo haya yakifanikiwa, msimu ujao Arsenal tutakuwa
kamili na tutacheza kushindania ubingwa pamoja na klabu kubwa zingine. Natambua
ugumu wa ligi ikizingatiwa kwamba klabu zingine zina makocha wapya, lakini, Arsenal
tutakuwa washindani wao wakubwa msimu ujao, na uzuri wa ligi ya England kabla ya ligi
kuisha mshindi hajulikani tofauti na Hispania ambapo mshindi ni Barcelona na
Madrid wakati wote’. Podolski ameyasema hayo huku hatua za usajili wa Higuain
na klabu ya Arsenal zikiwa kwenye hatua za mwisho mwisho na taarifa zinasema
Arsenal na Madrid wanatarajia kumalizana wakati wowote na Higuain atatua
Emirates.
No comments:
Post a Comment