Tuesday, June 4, 2013

Simba yajitoa CECAFA Kagame Cup

Uongozi wa klabu ya Simba umethibisha kutoshiriki kwenye michuano ya CECAFA Kagame Cup ikiwa michuano hiyo itafanyika nchini Sudan kama iliyopangwa. Kauli hiyo ya Simba imetolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo Mh. Aden Rage kwa kusema “klabu ya Simba haiwezi kwenda Darfur kwani hali ya usalama kwenye mji huo sio nzuri, na kauli ya serikali ya Sudan kuwa eneo hilo ni salama sio za kweli”. Simba itakuwa ni timu ya pili kujitoa kwenye michuano hiyo baada ya Al hilal na Al Merreikh kujitoa na taarifa zinasema klabu zingine zinategemea kujitoa pia kwenye michuano hiyo kutokana na sababu hiyo hiyo ya kiusalama. Mwishoni mwa wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje Mh Bernard Membe alithibitisha Bungeni kuwa hali ya usalama nchini Sudan sio nzuri na alishauri klabu za Tanzania kujitoa kwenye michuano hiyo. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 18 Juni hadi Julai 2 kwenye miji ya Darfur na Gordofan nchini Sudan, kufuatia hali hii wadau wengi wa soka wanategemea shirikisho la mpira wa miguu Afrika mashariki CECAFA kufanya maamuzi magumu ya kuhamisha michuano hiyo ili iweze kufanyika kwenye nchi nyingine. 

No comments:

Post a Comment