Tuesday, July 2, 2013

Vital’O mabingwa Cecafa Kagame Club Cup

Klabu ya Vital'O ya Burundi imefanikiwa kushinda kombe la Kagame mwaka huu baada ya kuifunga APR ya Rwanda magoli 2-0 katika mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa El Fasher uliopo kaskazini mwa Darfur. Pichani ni Nahodha wa Vital'O Amisi Tambwe akinyanyua kombe juu kushangilia ubingwa wa kwanza wa Kombe la Kagame kwa klabu hii. Mshindi wa tatu kwenye michuano hii ya Afrika Mashariki ni klabu ya Al Merreikh ya Sudan ambayo iliifunga klabu ya Rayon Sport ya Rwanda goli 1-0.  

No comments:

Post a Comment