Thursday, August 22, 2013

Bale avunja rekodi ya usajili, atua Madrid kwa £84mil

Hatimaye klabu ya Real Madrid imekubaliana na Tottenham Spurs juu ya uhamisho wa Gareth Bale kwa malipo ya paundi mil 84. Usajili huu wa Bale umevunja rekodi iliyowekwa na Cristiano Ronaldo mwaka 2009 aliposajiliwa na Madrid akitokea Man utd kwa paundi mil 80. Magazeti ya Skysport na Marca yamesema Gareth Bale anatarajiwa kutangazwa rasmi ijumaa ya wiki hii, na atatambulishwa rasmi mbele ya mashabiki wa Real Madrid wiki ijao. Usajili wa Bale unaendelea kuthibitisha nguvu za klabu ya Real Madrid ambayo imekuwa ikionesha misuli ya usajili wa mchezaji yoyote inayomuhitaji dhidi ya klabu mbalimbali duniani na inafanikiwa kumsajili kwa gharama yoyote. Klabu ya Real Madrid ndiyo inashikilia rekodi ya usajili wa wachezaji ghali kuliko klabu yoyote duniani tokea mwaka 2000. Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na Madrid na kuvunja rekodi ya usajili tokea mwaka 2000 ni Luis Figo (37mil) alitokea Barcelona, Zinedine Zidane (53mil) alitokea Juventus, Kaka (56mil) alitokea Ac Milan na Ronaldo (80mil) alitokea Man utd.       

No comments:

Post a Comment