Thursday, August 8, 2013

Barca yatuma ofa kumsajili Agger wa Liverpool

Wanted man: Agger is being chased by Spanish giants Barcelona after they were rebuffed in a bid for Luiz
Klabu ya Barcelona imetuma maombi rasmi ya kumsajili beki wa Liverpool, Daniel Agger kwa dau la paundi mil 17. Barcelona wamepeleka maombi haya kwa Liverpool baada ya kutolewa nje na klabu ya Chelsea kumsajili David Luiz. Barcelona wanatarajia kupata majibu kutoka kwa uongozi wa Liverpool wikiendi hii, lakini taarifa za awali alizozitoa kocha wa Liverpool Brendan Rodgers zinasema, hakuna mchezaji mzuri wa Liverpool atayeruhusiwa kuondoka msimu huu, kwani leng kuu la klabu ya Liverpool msimu ujao ni kuwa na kikosi bora ili kurudisha heshima yake.

Ofa hii ya Barca imesemekana kumchanganya kocha wa Liverpool Rodgers kwani ofa imekuja wakati joto la Luis Suarez kuondoka likiwa bado kali ikizingatiwa pia Agger mwenyewe ameonesha nia ya kutaka kujiunga na Barcelona.  

No comments:

Post a Comment