Friday, August 2, 2013

Liverpool yapeleka ofa Atletico kumsajili Diego Costa

Targeted: Atletico Madrid's Diego Costa could become Liverpool's latest signing
Sportsmail linaripoti klabu ya Liverpool imepeleka maombi kwa klabu ya Atletico Madrid ili kumsajili mshambuliaji wake Diego Costa. Liverpool imetajwa kulipa kiasi cha paundi mil 22 kwa mchezaji huyu, ofa ambayo inatarajiwa kutolewa maamuzi ndani ya siku chache. Ripoti zinasema klabu ya Liverpool imekataa kuongelea suala hili, kwani hawataki kuhusisha usajili wa mchezaji huyu na kuondoka kwa Luis Suarez. Lakini kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema ' kama tutafanya usajili wowote kwenye nafasi ya ushambuliaji lengo litakuwa ni kuimarisha safu hiyo kwani Suarez amefungiwa kucheza mechi sita za mwanzo na Daniel Sturridge bado ni majeruhi, hivyo hakutakuwa na mahusiano yoyote na Suarez'.  

No comments:

Post a Comment