Tuesday, October 22, 2013

Ferguson atoa kitabu cha historia yake kwenye soka

Unveiling: Sir Alex Ferguson holds his new autobiography in west London on Tuesday afternoon
Sir Alex kocha wa zamani wa Man utd akionesha kitabu chake alichokizindua leo. Ndani ya kitabu hiki kuna mambo mengi yahusuyo soka katika kipindi chote alichokuwa kocha wa klabu ya Man utd. Pia ameongelea baadhi ya wachezaji na wadau wa soka aliyowahi kukutana nao na kufanya nao kazi. Baadhi ya wachezaji na wadau aliowaongelea ni kama ifuatavyo; 


1. Cristiano Ronaldo: Amemtaja kama mchezaji mwenye kipaji kuliko wote aliyowahi kuwafundisha 
2. Beckham: Ni mchezaji mwenye tabia mbaya alikuwa anajisikia mkubwa kuliko kocha
3. Rooney: Alimuomba Sir Alex kutaka kuhama Man utd mwishoni mwa msimu uliopita 
4.  Owen Hargreaves: Sir Alex amemtaja mchezaji huyu kuwa ni usajili mbovu aliyowahi kuufanya kuliko wote
5. FA: Sir Alex amesema chama cha soka cha England kilishawahi kumuomba aifundishe timu ya taifa mara mbili akagoma
6. Rafa Benitez: Amemtaja kuwa ni kocha mwenye tabia ya hovyo na asiyeeleweka 
7. Roy Keane: Sir Alex amesema, hali ya maelewano ilikuwa njema ndani ya klabu baada ya Keane kuondoka Man utd, kwani amemtaja mchezaji huyu kuwa ni mkorofi na majibizano. 

Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyomo ndani ya kitabu, kwa bahari zaidi kuhusu kitabu hiki na yaliyomo unaweza kutembelea hapa bofya
Wantaway: Ferguson reiterates his claim that Wayne Rooney sought to leave the club before his retirement
Ouch: Beckham was left scarred after Ferguson kicked a boot at the former England captain
Worst ever? Owen Hargreaves (right) came under fire from Ferguson too for his lack of determination
Ronaldo at Real Madrid  Cristiano Ronaldo during his time at Sporting Lisbon

No comments:

Post a Comment