Monday, October 7, 2013

Kushinda vikombe sio kipaumbele Chelsea - Jose

Chelsea magazineKocha wa Chelsea Jose Mourinho wiki hii amefunguka kuelezea mpango wa klabu ya Chelsea ambao ulimfanya mmliki wa klabu hiyo Roman Abramovich kumrudisha kundini. Akielezea mpango huo kupitia vyombo vya habari vya klabu, Mourinho alifafanua kwa umakini mpango huo ili aweze kueleweka kwa wadau na washabiki wa soka. 'Mwanzo nilipokuja, uongozi wa klabu ulikuwa na mpango wa kuifanya klabu kushinda vikombe vingi ili kujenga jina na uwezo wa klabu kupambana ndani na nje ya England. Mpango huo ulifanikiwa kwa kiwango kikubwa na kwa miaka mingi. Baada ya mpango huo kufanikiwa kwa kushinda vikombe vingi, klabu ya Chelsea sasa inahitaji kufanikisha mpango mwingine ndiyo maana Abromovich amenileta. Mpango wa sasa wa klabu ni kujenga aina ya uchezaji ambao utaitambulisha klabu tofauti na zingine. Mpango huu hauna maana ya kupigania ubingwa wowote. Ikitokea tumeshinda kombe la ligi, basi itakuwa vyema zaidi, ila lazima watu wajue kushinda sio lengo letu la kwanza. Kujenga aina ya uchezaji sio jambo dogo, itachukua muda na wadau lazima watambue hilo. Mpango huu umeanzia kwa baadhi ya wachezaji, wakishaujua vyema watafundisha wengine na utasambaa kwa vijana na watoto waliopo ndani na nje ya klabu'. Hayo ndiyo maneno ya Jose Mourinho akielezea mpango mpya wa klabu hiyo, mpango ambao ulikuwa haujulikani na idadi kubwa ya wadau na washabiki wa Chelsea. Washabiki wengi wameupokea kwa furaha mpango huu, lakini wengine hawajaupenda kwa kile kilichosemekana sio vyema kusema kushinda vikombe sio kipaumbele kikubwa kuliko kujenga aina ya uchezaji. Katika kutetea hoja yao, washabiki hao walionekana kuwa na hofu na mpango huo, wakisema unaweza kufanya klabu ipoteze umaarufu wake kwa kukaa muda mrefu bila vikombe wakitolea mfano klabu ya Arsenal. Lakini wapo washabiki wengine waupenda mpango huo, kwani utaifanya Chelsea itambulike kwa aina yake ya uchezaji kama ilivyo kwa klabu ya Barcelona ambayo inajulikana kwa aina yake ya uchezaji duniani pote. All the best Mourinho and Chelsea FC  
New breed: Eden Hazard epitomises how Chelsea's style of play has evolved since Mourinho's first spell

No comments:

Post a Comment