Sunday, March 16, 2014

Yanga wanusurika kupata ajali mkoani Morogoro

Basi la klabu ya Yanga likiwa kwenye mtaro baada ya kunusurika kuanguka kwenye barabara ya Moro - Dar eneo la Mikese. Basi hili lilingia mtaroni baada ya mabasi yaliyokuwa yakitokea Dar kutanua na kuziba njia, jambo lililomfanya dereva wa basi la Yanga kuwapisha na kuingia mtaroni. Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa na tayari wachezaji wa Yanga na viongozi wamepata usafiri wa basi jingine kuelekea jijini Dar es salaam . Wachezaji na viongozi wa klabu ya Yanga waliokuwa wakitoka mjini Morogoro kucheza mechi dhidi ya Mtibwa jana jioni, mechi iliyokwisha kwa droo. 

Wachezaji wa Yanga na Viongozi wakitoka ndani ya basi kupitia kwenye madirisha

Name:  yanga.jpg
Views: 0
Size:  33.9 KB
Name:  yanga.jpg
Views: 0
Size:  16.9 KB\

No comments:

Post a Comment