Wednesday, October 23, 2013

Steve G ni bora kuliko wachezaji pendwa wa Sir Alex

Gerrard
Katika mahojiano na waandishi wa habari kuhusu kitabu chake alichokizindua wiki hii, kocha wa zamani wa Man utd Sir Alex Ferguson alisema wachezaji wa Man utd, Ryan Giggs na Paul Scholes ni wachezaji wazuri kuliko nahodha wa Liverpool Steven Gerrard. Baada ya kuongea hayo wachambuzi wa soka walipitia rekodi zilipo za wachezaji hawa watatu wakagundua kuwa Gerrard bado ni mchezaji bora zaidi yao. Ukiangalia takwimu zilizipo hapo chini utaona kuwa Gerrard amecheza mechi chache kuliko Giggs na Scholes lakini magoli aliyofunga na pasi alizotoa zinakaribiana na wachezaji hawa wa Man utd, jambo ambalo linaonesha pindi Gerrard akifikisha idadi ya mechi walizocheza Giggs na Scholes ni wazi kuwa ataweza akuwafikia au kuwazidi kwenye magoli na pasi za magoli. Mbali ya kumponda Steve G, kocha Alex Ferguson pia alishawahi kumhitaji mchezaji huyu mara kadhaa ili asajiliwe na Man utd ila mchezaji mwenyewe aligoma. 

Stats don't lie: Gerrard is on course to outscore Scholes and already has more assists, despite playing fewer Premier League games

Icon: Steven Gerrard has scored 100 Premier League goals from the Liverpool midfield

No comments:

Post a Comment