Friday, December 27, 2013

Diego Costa haondoki Atletico Madrid - Jose Luis

Not interested? Atletico Madrid director of football Jose Luis Caminero is confident Diego Costa (left) is not interested in a January move
Mkurugenzi wa soka wa klabu ya Atl. Madrid, Jose Luis Caminero amesema mshambuliaji wa klabu hiyo Diego Costa hana mpango wa kuhamia klabu za Arsenal na Chelsea ndani ya dirisha dogo. Caminero ameliongelea hilo mbele ya waandishi wa habari ili kuondoa tetesi zilizopo kuwa Costa ataihama Atl. Madrid mwezi January. Hadi sasa Diego Costa ameshafunga magoli 19 kati ya mechi 17 alizocheza na ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa magoli kwenye ligi ya Hispania. Kiwango alichokionesha Diego ndani ya msimu huu ndiyo kimemfanya apande chati na kuwa moja wa washambuliaji walipo kwenye soko. Mchezaji huyu ni raia wa Brazil lakini amebadilisha uraia na kuikana Brazil ili aweze kuichezea Hispania kwenye kombe la dunia. 

No comments:

Post a Comment