Klabu ya Arsenal imefikia hatua ya mwisho kumsajili mshambuliaji wa Schalke 04, Julian Draxler. Taarifa kutoka Sportsmail zinasema, klabu ya Arsenal imeshakubaliana na klabu yake pamoja na wakala wa mchezaji huyu, kilichobakia sasa ni ada ya uhamisho. Klabu ya Arsenal imetoa paundi mil 30 wakati klabu ya Schalke inahitaji paundi mil 37. Makubaliano baina ya klabu hizi yameonekana kuwa yataweza kukamilika siku yoyote kabla ya wikiendi hii. Tayari Draxler amewaeleza rafiki zake kuwa anahamia klabu ya Arsenal na ameonekana jijini Munich kwa daktari aliyemfanyia vipimo Ozil kabla ya kujiunga na Arsenal.
Kiungo wa Newcastle, Yohan Cabaye akiweka saini ya kuhamia klabu ya PSG ya Ufaransa kwa paundi mil 23. Cabaye amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu.
Sportmail linaripoti kuwa klabu ya Bayern Munich inajiandaa kumsajili beki wa Chelsea, David Luiz mwishoni mwa msimu huu. Pep Guardiola alishawahi kumuhitaji mchezaji huyu tokea alipokuwa akiifundisha klabu ya Barcelona na sasa akiwa Bayern Munich ameendelea kuonesha nia yake ya kumsajili Luiz, hivyo mwishoni mwa msimu huu inawezekana Luiz akajiunga na Munich.
Yevhen Konoplyanka (Katikati) amepamba vichwa vya habari za michezo nchini Uingeraza akihusishwa kuhamia Liverpool. Mchezaji huyu raia wa Ukraine aliyefunga moja ya goli zuri dhidi ya England kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia, ametajwa kumvutia kocha wa Liverpool, Braden Rodgers, na imesemekana kuwa atasajiliwa kwa paundi mil 20. Oleg Konoplyanka ambaye ni baba wa mchezaji huyu amethibitisha habari hizi akisema ' ni kweli mtoto wangu yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Liverpool naamini watafikia makubaliano ndani ya siku chache'. Yevhen ana umri wa miaka 24 anacheza nafasi ya pembeni (winga) kwenye klabu ya Dnipro nchini Ukraine.
Wakiwa kwenye harakati za kuziba pengo la Robert Lewandowski atakayejiunga na Bayern Munich msimu ujao, klabu ya Borussia Dortmund ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Man city, Edin Dzeko. Marca limeripo kuwa Man city na Dortmund bado wapo kwenye mazungumzo na muafaka wa uhamisho wa Dzeko unaweza kufikia tamati muda wowote na hivyo Dzeko kuhama ndani ya dirisha dogo au mwisho wa msimu.
Mchezaji wa Bayern Munich, Toni Kroos amesema yupo tayari kujiunga na Man utd kama klabu yake itakubali ahame. Toni ameeleza hayo akinukuliwa na Skysport akisema ' mimi moyo wangu ni mweupe kuhama, kila kitu nimewaachia Bayen Munich kwani wao ndiyo waajiri wangu hadi mwaka 2015. Kama watakubaliana na Man utd mimi nitaondoka bila shaka lolote'. Wakala wa mchezaji huyu ameshakutana zaidi ya mara moja na Moyes kwa mazungumzo na kilichobakia hivi sasa ni makubaliano kati ya Man utd na Bayern Munich tu.
Hii ni post ya akaunti rasmi ya Twitter ya klabu ya Man utd inayothibitisha kuwa klabu ya Manchester United itasajili wachezaji wengine wenye majina kama Juan Mata
The Sun limehabarisha, kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anatarajiwa kusaini mkataba mpya hivi karibuni. Habari zinasema Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Arsenal, Ivan Gazidis amethibitisha kuwa Wenger atasaini mkataba wa paundi mil 8 kwa mwaka na utakuwa ni mkataba wa miaka mitatu wenye jumla ya paundi mil 24.
Klabu ya Inter Milan imemetuma ofa kwa klabu ya Man utd ya kutaka kumsajili kwa mkopo winga Luis Nani. Taarifa kutoka Italia zinasema tayari Luis Nani mwenyewe ameshakubali kujiunga na Inter kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Ofa hii ya Inter inatarajia kujibiwa na Man utd mapema iwezekanavyo ili kufanikisha usajili wa mchezaji huyu kabla ya wikiendi.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amefunguka kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wake Samuel Eto'o. Akiulizwa na waandishi wa habari kuwa Eto'o atabaki mwisho wa msimu au ataondoka, Mourinho alisema ' Samuel alipenda mwenyewe kuja Chelsea, aliniambia hajawahi kucheza ligi ya England na angependa kujiunga na Chelsea ili atengeneze historia ya kucheza ligi kuu ya England. Mwisho wa msimu huu atakuwa ameshafanikisha nia yake ya kucheza EPL, sasa siwezi kujua kama atabaki au ataondoka. Lazima mjue kuwa Eto'o hataki kushinda kombe lolote, hana haja na pesa au kuwa mchezaji bora, anachokifanya sasa hivi ni kufurahia maisha yake kwenye soka. Alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nilishamsikia akisema atamalizia historia yake ya soka kwenye klabu iliyomkuza Real Mallorca, kwahivyo mwisho wa msimu huu yeye ndiye ataamua kubaki au kuondoka, lakini mimi ningependa abakie kwasababu anatusaidia sana kama timu'. Eto'o mwenye umri wa miaka 34 ameshashinda vikombe vyote vya ligi za Italia na Hispania, alishawahi kuwa mchezaji bora wa Afrika na alishawahi kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment