Shirikisho la soka nchini
Uingereza leo kimethibitisha matumizi ya tekinologia ya kutambua goli “goal
line technology” ambayo itaanza kutumika kuanzia msimu ujao wa ligi. Maamuzi ya
matumizi ya teknologia hii yamefikiwa baada ya FA kufanya kikao na viongozi wa
timu zote 20 za ligi hiyo na kukubaliana. Kampuni moja ya Kiingereza ndiyo
imeshinda tenda hiyo ambapo itafunga kamera saba kwenye kila goli na gharama ya
kufunga teknologia hiyo kwenye kila kiwanja ni paundi 250,000 sawa na tsh mil
605. FA imesema teknologia hiyo itatumika kwenye viwanja vya ligi kuu tu,
viwanja vingine vitafungiwa teknologia hiyo miaka ijayo kwasababu gharama zake
ni kubwa.
Wakati FA wakianza kutumia
teknologia hiyo shirikisho la mpira wa miguu nchini Hispania limesema, Hispania
itaanza kutumia teknologia hiyo baada ya miaka mitatu ijayo licha ya FIFA
kuruhusu matumizi ya teknoligia hiyo kuanza kutumika duniani kote. FIFA itaanza
kutumia teknologia hiyo mwaka 2014 katika michuano ya kombe la dunia nchini
Brazil ikiwa ni majaribio ya matumizi ya teknologia hiyo.
Mjadala wa teknologia
ya kutambua goli ulipamba moto kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Afrika
kusini katika mechi kati ya Ujerumani na Uingereza baada ya refa kukataa goli
lililofungwa na Frank Lampard kwa madai kuwa hakuona kama limevuka mstari. Tukio
hilo ndilo liliamsha mjadala wa matumizi ya teknologia ya goli ambao
umeshabikiwa sana na chama cha mpira nchini Uingereza ili iweze kutumika, na uamuzi wa FA kuanza kutumia teknologia hii ni moja ya jitihada za FA kuishawishi FIFA na wanachama wake kuitambua na kuanza kuitumia jambo ambalo linaonesha kufanikiwa.
No comments:
Post a Comment