Monday, February 3, 2014

Chelsea yaipiga Man city, mbinu za Mourinho noma!

Manchester City 0 - 1 Chelsea (Ivanovic) 



Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuifunga Man city kwa goli 1 - 0 lililofungwa na Ivanovic katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza. Mourinho amefanikiwa kuwazuia Man city vilivyo kwenye mchezo huu akiwatumia Willian, Matic na Luiz kuharibu mashambulizi ya Man city. Yaya Toure mchezeshaji wa Man city aliweza kubanwa vyema na Willian na kushindwa kufanya chochote katikati ya dimba. Hazard pia alikuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Man city, kwani aliweza kuwatoka kiulani kila mara alipokuwa akishika mpira. Man city watajilaumu kwa kutumia vibaya nafasi walizozipata kwenye dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza. Wadau wengi walifikiria Mourinho atapanga kikosi cha kupaki basi (19 century), lakini mambo yalikuwa tofauti kwani chelsea ilicheza mchezo wa kushambulia. Hakika Willian, Luiz na Matic ndiyo mbinu kubwa Jose Mourinho aliitumia kwa ushindi dhidi ya Man city, wachezaji hawa wamecheza vyema sehemu ya kiungo na ukabaji. Kwa ushindi huu klabu ya Chelsea imefikisha pointi 53 ikiwa nafasi ya tatu, lakini ikifanana pointi na Man city. 

Lineups Man city vs Chelsea 

Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Navas, Demichelis, Toure, Silva, Dzeko, Negredo

Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Luiz, Matic; Hazard, Ramires, Willian, Eto’o

Hakika Mourinho hajapaki basi leo

Etihad kabla ya mechi kuanza


Man city wakiingia uwanjani




Chelsea 
View image on Twitter
Chelsea wakiingia uwanjani 



Wachezaji wa Chelsea wakiwa kwenye mitaa ya jiji la Manchester leo mchana kabla ya mechi 

No comments:

Post a Comment