Wednesday, January 15, 2014

Kocha mkuu wa Yanga aanza kazi na ushindi Uturuki

Kocha Mkuu mpya wa Young Africans Hans Van Der Plyum na kocha msaidizi Charles Mkwasa wakiwa kazini katika mechi dhidi ya Altay

Young Africans imemkaribish vizuri kocha mkuu mpya Hans Van Der Plyum leo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK iliyopo Ligi Daraja la pili nchini Uturuki katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo mchana katika viwanja vya Sueno eneo la Side Manavgat.

Kocha Hans ambaye aliwasili jana jioni na kuongea na wachezaji kwa pamoja kabla ya chakula cha usiku alisisitiza nidhamu, upendo na kujituma miongoni mwa wachezaji na benchi la ufundi kitu ambacho mpaka sasa amefurahishwa na ushirikiano anaopewa na wachezaji na viongozi kwa ujumla.

Ikiwa mechi yake ya kwanza kama kocha mkuu wa Young Africans Hans aliweza kukaka kwenye benchi pamoja na makocha Charles Mkwasa, Juma Pondamali, Hafidh Saleh na daktari wa timu Dr. Suphian Juma ambapo kwa pamoja kikosi kimeweza kuendeleza ushindi wa pili mfululizo. Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Altay SK 0 - 0 Young Africans, lakini dakika 90 za mchezo zilimalizika kwa Altay SK 0 - 2 Young Africans. Magoli ya Yanga yamefungwa na Didier Kavumbagu na Okwi. 

Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Altay SK

No comments:

Post a Comment