Tuesday, February 4, 2014

Messi ana nidhamu nzuri uwanjani kuliko Ronaldo

Cristiano Ronaldo mchezaji bora wa dunia mwaka 2013 ameendelea kuongeza idadi ya kadi nyekundu katika historia ya maisha yake kwenye soka hadi kufikia nane (8). Wakati Ronaldo akiwa na kadi nyekundu nane, mpinzani wake Lionel Messi hana kadi nyekundu hata moja tokea aanze kucheza mpira wa kulipwa. Ronaldo alipewa kadi nyekundu nne akiwa na Man utd na ameshapewa kadi nyekundu nne akiwa na Real Madrid. Kadi nyekundu za Cristiano zimetokana na kuleta ugomvi kwenye mchezo, kujiangusha na kucheza faulo za waziwazi kwa mabeki. Kwa upande wa kadi za njano Cristiano Ronaldo ana kadi 79 kati ya mechi 579 alizocheza akiwa na klabu ya Man utd, Real Madrid na timu ya taifa, wakati Messi ana jumla ya kadi za njano 29 akicheza mechi 372 akiwa na Barca pamoja na timu ya taifa. Tofauti ya kadi za njano kwa wawili hawa ni 50 ambayo ni idadi kubwa na mbaya kwa Cristiano kama mchezaji bora wa dunia. 

Messi akioneshewa kadi ya njano baada ya kumsukuma beki wa Madrid.

Kawaida Messi analalamika akipewa kadi ya njano kuonesha kuumizwa na maamuzi ya refa, jambo ambalo ni tofauti na CR7 kwani wakati mwingine huwa anapiga makofi akiwepa kadi ya njano kitendo kinachoonesha dharau kwa refa kama picha iliyopo chini..

CR7 akipiga makofi baada ya kupewa kadi ya njano jambo ambalo Messi hawajawahi kufanya. 

Cristiano akila red card kipindi akiwa na Man utd

Cristiano akimpiga kichwa kiungo wa Bilbao wikiendi hii 

No comments:

Post a Comment