Wachezaji wa Man utd wakiwa mazoezini pamoja na kocha mkuu David Moyes. Mazoezi haya ni ya mwisho mwisho kabla ya kukutana na Olympiacos usiku wa leo. United itaingia uwanjani ikiwa nyuma kwa magoli 2-0 baada ya kukubali kipigo kwenye mechi ya awali nyumbani kwa Olympiacos. Ili kupita kwenda hatua inayofuata United wanatakiwa kushinda magoli 3-0 jambo ambalo linawezekana kwa timu kama Manchester United. Washabiki na wachambuzi wengi wanakubali kuwa United ya sasa sio kama ya zamani, lakini wanaamini kuwa wachezaji waliopo kama kocha atachagua kikosi kizuri basi Olympiacos lazima walie. Uzito wa mechi ya leo unaongezeka zaidi baada ya taarifa kuanza kuzagaa kuwa kibarua cha kocha David Moyes kitakua kwenye joto kali kama United watashindwa kusongambele kwenye michuano hii. Hali hii inakuja kutokana na ukweli kwamba Man utd wamepoteza nafasi ya kushinda vikombe vyote ndani ya England na Uefa champions ndiyo kombe pekee lililobakia kwa Moyes kuonesha muujiza. Usikose kuangalia mechi ya leo saa nne dk 45 usiku.
No comments:
Post a Comment