Friday, April 4, 2014

Aaron Ramsey kurudi wikiendi hii dhidi ya Everton

Star return: Arsene Wenger has revealed Aaron Ramsey could return from injury as soon as Sunday
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo wake Aaron Ramsey anategemea kucheza kwenye mechi kati ya Everton na Arsenal inayotarajiwa kufanyika wikiendi hii siku ya jumapili. Ramsey aliyeumia tokea Desemba mwaka jana amekaa nje ya dimba kwa kipindi kirefu na kurudi kwake wikiendi hii kutaongeza nguvu ya safu ya ushambuliaji kwani hadi anaumia, Ramsey alikuwa ni mfungaji tegemezi wa Arsenal. Mbali ya Ramsey, Wenger amesema Nacho Monreal pamoja na Diaby pia wameanza mazoezi na wanatarajiwa kurudi dimbani hivi karibuni. Arsenal na Everton wamepishana pointi nne, Arsenal wakiwa na pointi 64 na Everton pointi 60, lakini Everton bado wana mchezo mmoja mkononi. Mechi hii dhidi ya timu hizi mbili itakuwa ni ya upinzani mkubwa kwani timu zote mbili zinashindana kupata nafasi ya kucheza klabu bingwa Ulaya. 

No comments:

Post a Comment