Sunday, April 13, 2014

Azam FC mabingwa wa ligi kuu Tanzania 2014

Timu ya Azam FC imefanikiwa kunyakua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara leo hii baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Mbeya City kwa magoli 2-1. Mchezo huo uliokuwa mkali na waushindani hadi mapumziko Azam FC walikuwa wanaongoza kwa goli moja lililofungwa na Gaudence Mwaikimba. Kipindi cha pili kilishuhudia Azam wanapata goli la pili huku Mbeya city wakipata goli moja la kufutia machozi. Kwa matokeo ya leo Azam Fc imefanikiwa kufikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Azam FC imebakiza mchezo mmoja itakaocheza na JKT Ruvu April 19. Hongera Azam FC 

No comments:

Post a Comment