Thursday, April 10, 2014

Mourinho hatapewa adhabu yoyote - UEFA

Back to his best: Mourinho was up to his old tricks again at Stamford Bridge on Tuesday night
Mourinho akiongea na Torres ndani ya uwanja mara tu baada ya Chelsea kupata goli la pili dhidi ya PSG, kitendo hiki kilikuwa si cha kawaida kwa kocha kuingia ndani ya uwanja kushangilia goli au kutoa maelekezo kwa wachezaji. Kutokana na kitendo hiki, vyombo vingi vya habari viliandika na kuhoji kuhusu tukio hili ndipo UEFA ikaamua kutoa ufafanuzi kwa kusema kitendo hicho ni cha kawaida kutokana na mazingira yake, hivyo Mourinho hawezi kuchukuliwa hatua zozote za kinadhamu. Alipoulizwa Mourinho mwenyewe kuhusiana na tukio hili alisema ' tulikuwa tunacheza kwa kushambulia dakika zote za mwisho, na sehemu kubwa ya wachezaji walikuwa washambuliaji kwasababu tulikuwa tunahitaji kufunga. Baada ya goli kuingia ilinibidi niwape maelekezo mengine wachezaji wangu ili waweze kubadilisha aina ya uchezaji na kulinda ushindi wetu'. 

Precaution: Mourinho pulls Schurrle up from the pile of players to offer his advice
Quiet word: Mourinho grabs Fernando Torres by the head and issues some instructions
Make way: The Chelsea manager pushes Andre Schurrle out of his path so he can get to another star

No comments:

Post a Comment