Caughtoffside jarida la UK limesema, Bosi wa Chelsea, Abramovich ameshamchoka Torres na ameweka kiasi cha paundi milioni 45 ili kumnunua Hulk mshambuliaji wa Zenit. Hulk ambaye ni Mbrazil amejiunga na Zenit hivi karibuni lakini ameonesha wazi mapenzi yake na Chelsea. Torres alijiunga na Chelsea mwaka 2011 kwa paundi 50 milioni na hadi sasa hajaonesha uwezo wake uliotarajiwa. Abramovich yupo tayari kuingia hasara hiyo kwa kumwachia Torres aondoke Chelsea mwishoni mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment