Sir Alex Ferguson amepigwa faini ya paundi 8,500 na UEFA baada ya kugoma kuongea na waandishi wa habari siku Madrid waliposhinda goli 2-1 dhidi ya Man Utd. Ferguson alipatwa na hasira baada ya winga wa Man utd Nani kupewa kadi nyekundu kwa kumfanyia rafu Arbeloa wa Madrid. Utaratibu wa UEFA, kocha anatakiwa kuongea na waandishi wa habari kabla na baada ya mchezo, lakini Sir Alex aligoma kuongea na waandishi baada ya mchezo, kwa kutokubaliana na maamuzi ya Nani kupewa kadi nyekundu. Pia, Nani amepewa adhabu kwa kufungiwa mechi moja na UEFA.
No comments:
Post a Comment