Kiungo mwenye
mapafu ya mbwa Abdulhalim Humud Gaucho huenda akasafiri kuelekea bondeni Afrika
ya Kusini wikiendi hii kufuatia kupata nafasi ya majaribio kwenye timu ya Jomo
Cosmos aliyowahi kuchezea Nteze John na Ally Shah siku za nyuma. Cosmos
inayomilikiwa na kocha wa zamani wa Bafana Bafana Jomo Sono imempa nafasi hiyo
Humud baada yakufanyiwa mipango na uongozi wa Azam FC katika kutekeleza sera
yake ya kutengeneza uwanja mkubwa kwa wachezaji wa kitanzania kwenye ligi
mbalimbali zinazoendeshwa kisasa. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Azam FC.
No comments:
Post a Comment