Luca Toni
mshambuliaji wa Fiorentina amekiri kuwa kocha wa zamani wa Barcelona Pep
Guardiola alimuomba ushauri kuhusu kuhamia Bayern Munich. Pep na Toni walikuwa
timu moja mwaka 2001 na 2003 walipokuwa wakichezea club ya Brescia. Guardiola
alimuomba ushauri Toni kwasababu alishachezea club ya Munich mwaka 2007 hadi
2010 na kuweza kushinda kombe moja la Bundes. Toni alisema “Pep
aliniita mahali na akaniuliza vipi Munich kukoje, vipi hali ya maisha
ndani ya club, nilimjibu vyema na uamuzi wake kwenda Bayern ulinipa furaha.
Pep Guardiola mwishoni mwa mwaka jana alifunga mkataba na Munich ambao utaanza
mwanzoni mwa msimu ujao. Fununu zinasema Pep ameshaomba fungu
kubwa la usajili na kuwataja wachezaji anaowahitaji akiwemo Suarez, Mata na
Naymer.
No comments:
Post a Comment