Raisi wa FIFA Sepp Blatter amesema kuanzia mwaka 2018 na baada ya fainali za kombe la dunia nchini Qatar, kura za kuchagua nchi itakayoandaa kombe la dunia zitapigwa na wawakilishi wa nchi zote wanachama wa FIFA tofauti na hivi sasa ambapo kura zinapigwa na watu 22 tu kutoka kwenye kamati kuu ya FIFA. Blatter amesema njia hiyo mpya ya kupiga kura itaondoa vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara kipindi cha upigaji kura. Pia alisema utaratibu huo mpya utawafanya wapenzi wengi wa soka kurizika na matokeo yatakayokuwa yanatolewa.
No comments:
Post a Comment