Kipa wa Arsenal Szczesny ameomba msamaha kwa kocha wake Arsene Wenger na kwa club yake ya Arsenal kwa tabia aliyoifanya baba yake mzazi kumropokea Wenger kuwa ndiyo chanzo cha mtoto wake kushuka kiwango. Baba wa Szczesny amefikia hatua hiyo baada ya Arsene Wenger kumuweka benchi Szczesny kwenye mechi nyingi na zaidi ni taarifa zilizopo kwenye vyombo vya habari kuwa Arsenal iko mbioni kusajili golikipa mwingine mwenye uzoefu zaidi. Szczesny amesema anaomba msamaha kwa kocha na club, vilevile alisisitiza kuwa alichokisema baba yake yeye hakiamini na yalikuwa mawazo tu kama ya mtu mwingine wa kawaida.
No comments:
Post a Comment