BBC inaripoti kuwa, bingwa mtetezi wa mashindano ya mbio za magari Sebastian Vettel ameshinda mbio za Malaysia Grand Prix licha ya kukaidi maagizo ya mabosi wake kampuni ya Red Bull. Vettel ambaye ameshinda mbio hizo mbele ya dereva mwenzake Mark Weber ambaye alikuwa akiongoza baada ya kituo cha mwisho,licha ya kupewa maagizo na mkuu wa Red Bull ya kukaa nyuma ili kumpisha Webber alionekana kufanya vizuri toka kuanza kwa mbio hizo zilizofanyika hii leo huko nchini Malaysia. Baada ya ushindi huo,Bosi wa Red Bull alisikika akimpongeza Vettel,lakini akimwambia ana kazi ya kujieleza zaidi kwa nini amekiuka maagizo ya Timu yake na kuanza kushindana na Dereva mwenzake kutoka Timu ya Red Bull. Sebastian Vettel mwenyewe ameomba radhi kwa kitendo hicho,huku akisema alikuwa hana jinsi kwani wote walikuwa wakishindana kushinda. Dereva Muingereza Lewis Hamilton alimaliza wa tatu mbele ya Nico Roseberg wa Timu yake ya Mercedes licha ya kujisahau na kusimama kwenye kituo kisicho kuwa chake kubadilisha matairi ya gari kwenye raundi ya mwisho ya mbio hizo.
No comments:
Post a Comment