Monday, March 25, 2013

TFF haitambui uongozi wa muda wa Simba


Mkutano Mkuu wa Dharura ulioitishwa na wanachama wa Simba, Machi 17 mwaka huu na kuuondoa uongozi wa klabu hiyo si halali kwa vile haukufuata taratibu, na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitambui kamati za Muda. Uamuzi huo umefikiwa na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Machi 24 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa. Kamati imebaini kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 22(2) ya Katiba ya Simba, Mkutano Mkuu wa Dharura unaitishwa na Kamati ya Utendaji baada ya wanachama wasiopungua 500 kuwasilisha ombi hilo kwa maandishi na kujiorodhesha, lakini mkutano huo haukuitishwa na Kamati ya Utendaji ya Simba hivyo ni batili. Taarifa hizi zimetolewa na TFF

No comments:

Post a Comment