Uwanja Mpya wa West Ham |
Club ya West Ham imekamilisha mipango yake ya kukodi uwanja wa taifa wa Olimpiki. Kiwanja hicho chenye uwezo wa kubeba watazamaji 80,000 kitakuwa kikitumiwa na West Ham kuanzia mwaka 2016/17. West Ham italazimika kulipia gharama za marekebisho ya awali na ada ya pango kila mwaka la paundi milioni 2. West Ham inatarajia kuongeza mapato zaidi pindi itakapohamia kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji mara mbili ya uwanja wanaotumia sasa.
No comments:
Post a Comment