Mshambuliaji wa Man City Sergio Aguero amemwomba radhi David
Luiz wa Chelsea baada ya kumfanyia rafu mbaya katika mchezo wa nusu fainali
kati ya Chelsea na Man city wikiendi iliyopita. Aguero alitakiwa kupewa kadi
nyekundu katika mchezo huo lakini mwamuzi hakuweza kutoa adhabu hiyo jambo
ambalo lilisababisha mzozo kwa mashabiki wa Chelsea lakini Aguero alitambua
makosa yake na amekiri kuwa alimfanyia rafu mbaya Luiz. Aguero alimuomba
msamaha Luiz kwa kumpigia simu na kukubaliana, baada ya kukubaliana kwenye
simu Aguero na Luiz walimalizia maongezi yao kwenye twitter ambapo Aguero alisema “Nimewasiliana
na Luiz na nimemuomba msamaha kwasababu nilifanya rafu ambayo sikukusudia” naye
Luiz alijibu kwa kusema “nakushukuru Aguero kwa ujasiri na utu ulioonesha”.
Mbali na msamaha alioupata Aguero kutoka kwa Luiz, FA pia imesema haitatoa
maamuzi yoyote kufuatia rafu hiyo kwani sio rafu ambayo ilikuwa inahitaji maamuzi
ya nje ya uwanja.
No comments:
Post a Comment