Timu ya Yanga leo imetoka droo ya goli moja kwa moja na timu
ya Mgambo katika mechi iliyofanyika katika uwanja wa mkwakwani jijini Tanga.
Kwa matokeo haya Yanga inaendelea kushika nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 53
licha ya kujipunguzia kasi kuelekea kwenye ubingwa wa ligi kuu. Kama Yanga
ingeshinda mechi ya leo ingebakiza pointi mbili tu ili kunyakuwa ubingwa, ila
kwa matokeo ya leo umeifanya Yanga ibakize pointi nne kuchukua ubingwa katika
michezo mitatu iliyobakia.
No comments:
Post a Comment