Cardiff imekuwa ni timu ya kwanza kuingia ligi kuu ya
Uingereza baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Charton katika mechi
iliyofanyika jana usiku. Cardiff imeweza kufikisha pointi 84 pointi ambazo
zinaweza kufikiwa na timu moja tu ya Hull City. Kutoka ligi ya
championship timu tatu tu ndiyo zinatakiwa kupanda daraja, hivyo timu moja imeshapatikana na zimebakia timu mbili ambapo hadi sasa mchuano mkali upo kwenye timu tatu za
Hull city, Watford na Brighton ambazo zinawania nafasi mbili zilibakia.
Ukiangalia msimamo kwenye jedwari hapo chini utaona tofauti ndogo ya pointi
kati ya timu hizi ambazo zimebakiza michezo mitatu kila mmoja. Cardiff yenye udhamini
wa 1Malaysia imeweza kuingia ligi kuu baada ya miaka 51 jambo ambalo ni la
kihistoria kwenye mji wa Cardiff City.
No comments:
Post a Comment