Ujumbe wa kamati ya FIFA umemaliza kazi yake ya kuchunguza mgogoro wa uchaguzi mkuu TFF na utatoa
majibu baada ya siku saba. Mkuu wa ujumbe huo bwana Primo Cavarro amesema wameyasikiliza maelezo
ya kila mgombea baada ya uchambuzi FIFA itatangaza majibu ya uchunguzi huo
majibu ambayo yatatoa misingi na maagizo yatakayo ongoza uchaguzi mkuu wa TFF.
Naye Rais wa TFF bwana Leodegar Tenga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mbele ya
ujumbe huo wa FIFA amesema anaamini mvutano uliokuwepo baina ya wagombea,
serikali na TFF umekwisha na maamuzi ya FIFA yataheshimiwa kwani wanauzoefu wa
maswala ya usuluhishi kwenye soka bila kupendelea upande wowote. Baada ya
kumaliza kazi yake ujumbe wa FIFA unatarajia kuondoka wiki hii kuelekea Zurich,
Uswisi yalipo makao makuu ya FIFA kuwasilisha taarifa ya uchunguzi walioufanya.
No comments:
Post a Comment